Ibn ´Uthaymiyn mdaiwa kuhiji baada ya kupata idhini ya mwenye deni lake

Swali: Ni upi usahihi wa yale yanayonasibishwa kwenu kwamba umesema:

“Mtu akiwa na deni na akamuomba idhini yule mwenye deni kufanya hajj basi hakuna neno juu yake.”?

Jibu: Hapana, hili si sahihi. Yule aliye na deni basi alipe deni la watu kwanza. Hata kama yule mwenye deni lake atampa idhini ya kufanya hajj bado hajj itakuwa si wajibu kwake. Kwa sababu akimpa idhini ya kufanya hajj, je, deni lake laanguka? Halianguki. Lakini mtu akiwa na deni dogo na anajua kuwa pindi atapopata mshahara wake mwishoni mwa Dhul-Hijjah ataweza kulilipa, katika hali hii ni sawa akahiji. Kwa sababu anaiamini nafsi yake. Ama madeni mengi bora ni kwa mtu kuyalipa kwanza kabla ya kuhiji.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/926
  • Imechapishwa: 17/11/2018