Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya Qadar ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ

”Hakika kila kitu Sisi Tumekiumba kwa makadirio.”[1]

MAELEZO

Dalili ya nguzo ya sita katika nguzo za imani ni maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ

”Hakika kila kitu Sisi tumekiumba kwa makadirio.”

Bi maana kila kilichoumbwa na Allaah kimekadiriwa katika elimu, uandishi na utashi Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Hakikutokea kiholela. Bali ni jambo limetangulia katika elimu ya Allaah, kimeandikwa katika ubao uliohifadhiwa na kimetangulia katika matakwa na utashi wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] 54:49

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 221
  • Imechapishwa: 26/01/2021