05. Maana ya Uislamu na kwamba ndio waliokuja nao Mitume wote

Uislamu ndio dini ya Mitume wote. Allaah (Subhaanah) amesema:

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ

 “Hakika dini mbele ya Allaah ni Uislamu.”[1]

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kutoka kwake, naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[2]

Uislamu katika zama za Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa ni kule kumwamini Allaah, kumwabudu Yeye pekee, kumpwekesha, kumwabudu Yeye pekee na kumsadikisha Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuyafuata yale aliyokuja nayo. Vivyo hivyo ndivo ilivokuwa wakati wa Huud, Swaalih, Ibraahiym na wale Mitume wengine wote waliokuja baada yao. Maana ya Uislamu ilikuwa ni kumwabudu Allaah pekee, kumtakasia Yeye nia na Ummah huo kumwamini Mtume wao ambaye ametumilizwa kwao na kuyafuata yale aliyokuja nayo. Kadhalika katika zama za Muusa na wale wengine waliokuja baada yake mpaka ilipofika zama za ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati Allaah alipomtuma Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi Uislamu ambao Allaah anauridhia ikawa ni yale ambayo Allaah amemtumiliza kwayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kuwamini, kumwabudu Yeye pekee, kumtakasia Yeye nia, kumwamini Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale aliyoteremshiwa katika Qur-aan na Sunnah pamoja na kuwaamini wale Manabii na Mitume wengine waliokuwa kabla yake. Kila ambaye atamfuata na akasadikisha yale aliyokuja nayo basi ni katika waislamu. Na yule atakayejiepusha na hayo baada ya kwamba umekwishamfikia ulinganizi basi yeye ni katika makafiri.

[1] 03:19

[2] 03:85

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/articles/78/الاسلام-هو-دين-الله-ليس-له-دين-سواه
  • Imechapishwa: 06/10/2021