Ni lazima kwa waislamu kulingania katika haki, wafafanue Uislamu, mazuri yake na wabainishie ukweli wake kwa jamii zote kwa lugha wanazofahamu ili wafikiwe na ujumbe wa Allaah, Mtume na dini Yake. Vilevile ni lazima kwao kufichua hoja tata wanazobabaisha kwazo maadui wa Uislamu na wajibu matusi wanayotusi maadui wa Uislamu na wabainishe ubatilifu wake kwa dalili za Qur-aan na Sunnah na za kiakili. Kwani Allaah amewalazimu kuinusuru dini na Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akawaeleza (Subhaanah) kwamba hakuna uokozi wala kufaulu isipokuwa kwa yule mwenye kuinusuru haki na akaifuata.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/articles/78/الاسلام-هو-دين-الله-ليس-له-دين-سواه
  • Imechapishwa: 06/10/2021