Swali: Je, ngazi hizi zinalingana upande wa thawabu za kisomo cha Qur-aan, vita na swadaqah?

Jibu: Thawabu zinatofautiana kutegemea nia ya mja, utakasifu wake, ukweli wake na ukamilifu wa kitendo chake. Kwa hiyo inatofautiana. Huyu anaswali na mwingine anaswali hata hivyo kati ya swalah hizo mbili kuna utofauti kama utofauti wa mashariki na magharibi. Huyu wa kwanza ameielekea swalah yake, akaitilia umuhimu, akamnyenyekea Allaah na akaikamilisha. Huyu wa pili ameifanyia upungufu. Kwa hiyo kati yazo kunakuwa na tofauti. Vivyo hivyo swawm zao na hajj zao zinatofautiana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21903/هل-تتفاوت-درجات-الثواب-للاعمال-الصالحة
  • Imechapishwa: 29/09/2022