Zaynab bint Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

Yeye ndiye alikuwa mkubwa wa kina mama wa wale waliohajiri.

Alimuoza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa binamu yake Abul-´Aasw kipindi cha uhai wa mama yake. Akamzalia Umaamah, ambaye aliolewa na ´Aliy bin Abiy Twaalib baada ya kufariki kwa Faatwimah, na ´Aliy bin Abiyl-´Aasw. Inasemekana kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkaza juu ya kipando nyuma yake wakati wa kufunguliwa mji wa Makkah. Nadhani kuwa alikufa akiwa mdogo.

Zaynab alisilimu na akahajiri kabla ya kusilimu kwa mume wake kwa miaka sita.

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituma kikosi na mimi nilikuwa mmoja wao. Akasema: ”Mkikutana na Habbaar bin al-Aswad na Naafiy´ bin ´Abd, basi wachomeni moto. Wote wawili walikuwa wamemchezea shere Zaynab wakati alipotoka na akapatwa na maradhi ya ulemavu mpaka alipokufa.” Baadaye akasema: ”Mkikutana nao, basi waueni. Haitakikani kwa yeyote kuadhibu kwa adhabu ya Allaah.”[1]

Yaziyd bin Marwaan amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha watu swalah ya asubuhi. Alipoanza kuswali, Zaynab akaita: ”Mimi nimempa ulinzi Abul-´Aasw bin ar-Rabiy´.” Alipomaliza swalah yake, akasema: ”Mimi sikujua hilo. Wale watu wa chini kabisa wana haki ya kutoa ulinzi.”[2]

ash-Sha´biy amesema:

“Zaynab aliingia katika Uislamu na akahajiri. Kisha yeye [mumewe] akasalimu baada ya hapo na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwateganisha.”[3]

Hivo pia ndivo alivosema Qataadah na akaongeza:

“Halafu kukateremshwa Suurah “at-Tawbah”. Mwanamke akisilimu kabla ya mume wake, basi hana haki yoyote juu yake isipokuwa kama atamwacha huru.”

Ibn ´Abbaas amesema:

“Baada ya miaka mingi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimrudisha msichana wake Zaynab kwenda kwa Abul-´Aasw kujengea kwa ile ndoa ya mwanzo. Hakukuwa na haja ya mahari mapya.”[4]

Alifariki mwanzoni mwa mwaka wa 08.

Umm ´Atwiyyah amesema:

“Wakati alipofariki Zaynab, msichana wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), alisema: “Mwosheni na muwitirishe; mara tatu au tano, na mjaalie mara ya mwisho kafura au kitu katika kafura. Mtapomaliza basi nijuzeni. Tulipomaliza tukamjuza ambapo akatutupia kikoi chake na akasema: “Msitirini kwacho.”[5]

[1] Shu´ayb al-Arnaa’uutw amesema:

”Cheni ya wapokezi wake ni yenye nguvu.”

[2] Ibn Hishaam (1/157). Shu´ayb al-Arnaa’uutw amesema:

”Wanaume wake ni waaminifu.”

[3] at-Twabaqaat al-Kubraa (8/32).

[4] Ibn Hishaam (1/658). Shu´ayb al-Arnaa’uutw amesema:

”Swahiyh.”

[5] Muslim (939).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (2/246-250)
  • Imechapishwa: 06/10/2020