Acha kupika nguruwe kama we ni mkweli juu ya Uislamu wako

Swali: Nafanya kazi ya upishi katika shirika moja la kigeni na hupika pia nyama ya nguruwe licha ya kwamba najua hakika juu ya uharamu wake. Pamoja na hivyo siionji na wala siwahudumii nayo wafanya kazi waislamu. Je, napata dhambi kwa kuipika na kuwahudumia wafanya kazi wa kigeni?

Jibu: Ndio, haifai kwako kufanya hivo. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Saidianeni katika wema na kumcha Allaah na wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”[1]

Kupika nguruwe na kuwahudumia wageni au waliokupa kazi hiyo ni maovu na ni kusaidia maovu. Kwani Allaah ameharamisha kwao nguruwe kama alivyoiharamisha kwa waislamu. Kwa hivyo haifai kwako kuwasaidia juu ya yale aliyoharamisha Allaah. Ni kama ambavo haifai kwako kuwasaidia juu ya shirki na kumwabudu ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuwasaiida kunywa pombe na maasi mengine. Vivyo hivyo haifai kwako kuwasaidia kupika nguruwe, kuwahudumia wao au wageni. Yote haya ni maovu. Kwa hiyo ni lazima kwako kutahadhari juu ya jambo hilo, kujikwamua na kujitenga nao mbali kama kweli wewe ni mkweli juu ya Uislamu wako.

[1] 05:02

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/9181/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B7%D8%A8%D8%AE-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B3%D9%84%D9%85-%D9%84%D8%AD%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%AE%D9%86%D8%B2%D9%8A%D8%B1-%D9%84%D8%BA%D9%8A%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B3%D9%84%D9%85%D9%8A%D9%86