Swali: Je, inakubaliwa swadaqah au zawadi ya mla ribaa?
Jibu: Ikiwa mali zake zote ni za ribaa, hapana, haikubaliki. Lakini ikiwa anayo biashara au shughuli nyingine pamoja na zile za ribaa, basi hapana tatizo. Ni kama vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyonunua chakula kutoka kwa mayahudi ambao wanajishughulisha na kula ribaa, kwa sababu walikuwa wakila ribaa lakini pia walikuwa na shughuli nyingine halali. Lakini mtu ambaye hana kipato kingine isipokuwa cha ribaa pekee, basi hapana. Haikubaliki kufanya naye muamala.
Swali: Mtu mwenye mali iliyochanganyika baina ya halali na haramu – je, anapaswa kuwa na khofu ya kutokukubaliwa?
Jibu: Aliyechanganya mali yake baina ya halali na haramu, hakuna tatizo kufanya naye muamala. Hata hivyo mtu huyo anapaswa kumcha Allaah na ajiepushe.
Swali: Je, anapaswa kuogopa kwamba du´aa zake hazitakubaliwa?
Jibu: Ndio, kula ribaa na mali ya haramu ni miongoni mwa sababu za kutokukubaliwa kwa du´aa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31351/هل-تقبل-هدية-من-يتعامل-بالربا
- Imechapishwa: 21/10/2025
Swali: Je, inakubaliwa swadaqah au zawadi ya mla ribaa?
Jibu: Ikiwa mali zake zote ni za ribaa, hapana, haikubaliki. Lakini ikiwa anayo biashara au shughuli nyingine pamoja na zile za ribaa, basi hapana tatizo. Ni kama vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyonunua chakula kutoka kwa mayahudi ambao wanajishughulisha na kula ribaa, kwa sababu walikuwa wakila ribaa lakini pia walikuwa na shughuli nyingine halali. Lakini mtu ambaye hana kipato kingine isipokuwa cha ribaa pekee, basi hapana. Haikubaliki kufanya naye muamala.
Swali: Mtu mwenye mali iliyochanganyika baina ya halali na haramu – je, anapaswa kuwa na khofu ya kutokukubaliwa?
Jibu: Aliyechanganya mali yake baina ya halali na haramu, hakuna tatizo kufanya naye muamala. Hata hivyo mtu huyo anapaswa kumcha Allaah na ajiepushe.
Swali: Je, anapaswa kuogopa kwamba du´aa zake hazitakubaliwa?
Jibu: Ndio, kula ribaa na mali ya haramu ni miongoni mwa sababu za kutokukubaliwa kwa du´aa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31351/هل-تقبل-هدية-من-يتعامل-بالربا
Imechapishwa: 21/10/2025
https://firqatunnajia.com/zawadi-na-swadaqah-ya-mla-ribaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket