64 – al-Baraa´ bin ´Aazib (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia: “Unapotaka kitandani mwako, basi tawadha wudhuu´ kama wa swalah kisha lalia ubavu wa kulia kisha useme:
اللّهُـمَّ أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت
”Ee Allaah! Nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, nimeyaegemeza mambo yangu Kwako, nimeuelekeza uso wangu Kwako, nimeutegemeza mgongo wangu Kwako hali ya kuwa ni mwenye kukutarajia na mwenye kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa isipokuwa Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako ulichokiteremsha na Nabii Wako Uliyemtuma. Akifa basi amekufa juu ya maumbile. Yafanye hayo ndio ya mwisho unayosema.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Imekuja katika tamko jengine:
اللهم أسلمت وجهي إليك
“Ee Allaah! Nimeusalimisha uso wangu Kwako… “
Imekuja katika tamko jengine tena:
اللهم أسلمت نفسي إليك، ووجهت وجهي إليك
“Ee Allaah! Nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, nimeulekeza uso wangu Kwako… “[2]
MAELEZO
Dhikr hii ni tukufu na ndani yake kuna kutangaza imani ya kumwamini Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndani yake kuna kumwelekea Allaah (´Azza wa Jall), kumdhalilikia, kumtegemea, kujisalimisha na hukumu Yake, kunyenyekea Shari´ah Yake, kuamini mipango na makadirio Yake na Kitabu Chake na Mtume Wake. Kwa ajili hiyo ndio maana ikawa na thawabu hizi ya kwamba mwenye kuyasema kisha akafa katika usiku huo, basi amekufa juu ya maumbile. Ndani yake kuna fadhilah za Dhikr hii. Ndani yake kuna fadhilah za muislamu kulala na twahara. Ndani yake kuna mapendekezo ya kulalia ubavu wa kulia na pia aweke mkono wake wa kulia chini ya shavu lake la kulia. Ndani yake kuna ya kwamba haitakiwi kubadilisha matamshi ya Adhkaar wala kuyasimulia kimaana. Bali mtu anatakiwa kuyasema kwa matamshi yake kama yalivyopokelewa. Ndani yake kuna ya kwamba Dhikr ndio ya mwisho inayosemwa wakati wa kulala.
[1] al-Bukhaariy (6311) na Muslim (2710).
[2] al-Bukhaariy (6315) na Muslim (2710).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 72-73
- Imechapishwa: 22/10/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 72-73
Imechapishwa: 22/10/2025
https://firqatunnajia.com/08-dhikr-ya-mwisho-inayosemwa-kabla-ya-kulala/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket