Swali: Ni ipi hukumu ya zawadi katika Uislamu? Je, inakubaliwa au inakataliwa?
Jibu: Msingi wa zawadi ni kwamba inakubaliwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikubali zawadi na alikuwa akilipa kwa ajili yake. Ameipokea al-Bukhaariy kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Isipokuwa ikiwa zawadi ni kama malipo ya dini yake: mfano anayopewa hakimu ili atende dhuluma, khiyana au asipitishe haki au anayopewa mfanyakazi ili afanye khiyana, hiyo asiipokee. Zawadi zinazotolewa kwa wafanyakazi ili wasitoe haki huwa ni rushwa.
Kuhusu zawadi katika asili yake ni jambo la kheri, kujikurubisha na ni miongoni mwa sababu za kuleta mapenzi. Lakini inapasa yule aliyekabidhiwa zawadi kulipa kwa kumpa zawadi pia, ili kulinganisha na zawadi aliyopewa, ikiwa ni katika mlango wa zawadi. Ama ikiwa ni katika mlango wa swadaqah, basi hiyo ina hukumu nyingine tofauti.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30121/ما-حكم-الهدية-في-الاسلام
- Imechapishwa: 12/09/2025
Swali: Ni ipi hukumu ya zawadi katika Uislamu? Je, inakubaliwa au inakataliwa?
Jibu: Msingi wa zawadi ni kwamba inakubaliwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikubali zawadi na alikuwa akilipa kwa ajili yake. Ameipokea al-Bukhaariy kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Isipokuwa ikiwa zawadi ni kama malipo ya dini yake: mfano anayopewa hakimu ili atende dhuluma, khiyana au asipitishe haki au anayopewa mfanyakazi ili afanye khiyana, hiyo asiipokee. Zawadi zinazotolewa kwa wafanyakazi ili wasitoe haki huwa ni rushwa.
Kuhusu zawadi katika asili yake ni jambo la kheri, kujikurubisha na ni miongoni mwa sababu za kuleta mapenzi. Lakini inapasa yule aliyekabidhiwa zawadi kulipa kwa kumpa zawadi pia, ili kulinganisha na zawadi aliyopewa, ikiwa ni katika mlango wa zawadi. Ama ikiwa ni katika mlango wa swadaqah, basi hiyo ina hukumu nyingine tofauti.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30121/ما-حكم-الهدية-في-الاسلام
Imechapishwa: 12/09/2025
https://firqatunnajia.com/zawadi-katika-uislamu/