Zamu kwa mwenye hedhi na mwenye nifasi

Swali 832: Ni lazima kuwagawia masiku mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi?

Jibu: Kilichotangaa kwenye madhehebu [ya Hanaabilah] ni ulazima wa kuwagawia masiku kwa wote wawili. Kwa sababu wote wawili ni wake. Lakini maoni sahihi yanayofanyiwa kazi ni kwamba mwanamke mjamzito anagawiwa siku. Kuhusu mwanamke mwenye damu ya uzazi hagawiwi zamu. Desturi ni yenye kupita hivo na kuridhia kwake kutogawiwa zamu. Bali mara nyingi mwanamke midhali ni mwenye nifasi hapendi kugawiwa zamu na mume wake, jambo ambalo lina mashiko fulani katika madhehebu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 328
  • Imechapishwa: 19/07/2019