Zakaah ya vyenye kutoka ardhini

Swali: Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema kuwa inatakiwa kutoa zakaah 1/5 kwa ajili ya vile vitokavyo ardhini, pasi na kujali ni mali aina gani na kiwango chake. Je, hiyo ina maana kwamba vile vyenye kuchimbwa kutoka ardhini havina kiwango ambacho ni lazima kinachozingatiwa (النصاب)?

Jibu: Ndio. Havina kiwango ambacho ni cha lazima, ni mamoja kiwango ni kikubwa au kidogo. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewajibisha kutoa 1/5 juu ya vile vinavyochimbwa na wala hakutoa maelezo kupambanua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 27/04/2021