Swali: Je, katika mkopo kuna zakaah?

Jibu: Ndio. Mkopo unapokuja kwako na ukazungukiwa na mwaka basi unatakiwa kuutolea zakaah. Umeshakuwa na mali mikononi mwako. Ukikopa kutoka kwa Zayd 1000, 2000, 100 000 au zaidi na pesa hiyo ikazungukiwa na mwaka nayo ipo kwako, basi unatakiwa kuzitolea zakaah. Kwa sababu ni mali yako na imekuwa deni juu yako kwa ndugu yako. Hivyo unatakiwa kutoa zakaah yake kama unavyotoa zakaah ya mali nyingine ulizopata kwa zawadi au kwa njia nyingine inayokubalika katika Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1058/هل-في-القرض-زكاة
  • Imechapishwa: 13/01/2026