Swali: Vipi kuhusu picha za TV?

Jibu: Ni katika mlango huu. Huenda ikasemwa kwamba kwa ajili ya manufaa makubwa, kwa maana kuwa manufaa yanapewa uzito kuliko picha, kwa mlango wa kuondoa madhara makubwa zaidi kwa kutenda lililo na madhara madogo, na kwamba hupimwa kwa upigaji picha wa wafanyakazi viwandani au kwenye mambo ambayo waislamu wanayahitaji na hupata uongofu kupitia hayo. Huenda ikasemwa kuwa hili liko katika mlango wa elimu, basi hupuuzwa yaliyomo ya taswira kwa ajili ya manufaa makubwa ya kujifunza mambo yenye umuhimu.

Ama kumpiga picha mwanamke, kumrekodi fulani na fulani kwa kujifurahisha tu, na filamu, hili si udhuru wa Kishari´ah. Huu si udhuru. Katika viwanda, tiba na yanayofanana na hayo, kwa mtazamo wa baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa inaingia katika mlango wa kutenda madhara madogo kwa kuzuia madhara makubwa. Lakini kupanua jambo hili katika darsa, kwenye TV au katika vitu vingine, sijui sababu ya Kishari´ah inayolifanya liwe halali, kwa sababu wamepanua jambo hili bila udhuru wa Kishari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1052/حكم-التصوير-التلفزيوني
  • Imechapishwa: 13/01/2026