Zakaah ni miongoni mwa amri za Mola kwa Mitume Yake mwa mujibu wa Biblia II

25Mwenyezi Mungu akaongea na Mose akamwambia: 26”Wewe na mchungaji Eleazari, pamoja na viongozi wa koo za jumuiya ya Waisraeli, fanyeni hesabu ya nyara ya vitu, watu na wanyama. 27Gaweni nyara katika mafungu mawili, fungu moja la wanajeshi waliokwenda vitani na fungu lingine kwa ajili ya jumuiya nzima. 28Kisha kutokana na lile fungu la wanajeshi waliokwenda vitani, tenga zaka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu: Kitu kimoja kutoka kila vitu 500, iwe ni watu, ng’ombe, punda, kondoo au mbuzi, 29umpe mchungaji Eleazari kuwa sadaka kwa Mwenyezi Mungu. 30Kutoka lile fungu la jumuiya nzima, chukua sehemu moja ya kila hamsini, iwe ni watu, ng’ombe, punda, kondoo na mbuzi. Hivyo utawapa Walawi ambao wana wajibu wa kuhudumu katika hema la Mwenyezi Mungu.” 31Mose na mchungaji Eleazari walifanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Mose. 32Nyara walizoteka wanajeshi zilikuwa: Kondoo 675,000, 33ng’ombe 72,000, 34punda 61,000, 35na wasichana ambao hawakuwa wamelala na mwanamume 32,000. 36Nusu yake, sehemu ambayo iligawiwa wanajeshi waliokwenda vitani, ilikuwa kondoo 337,500, 37katika hao 675 walitolewa kwa Mwenyezi Mungu. 38Ng´ombe wa wanajeshi walikuwa 36,000, na katika hao 72 walitolewa zaka kwa Mwenyezi Mungu. 39Punda wao walikuwa 30,500, na katika hao 61 walitolewa zaka kwa Mwenyezi Mungu. 40Watu walikuwa 16,000, na katika hao sehemu ya Mwenyezi Mungu ilikuwa ni watu thelathini na wawili. 41Basi, Mose akampa mchungaji Eleazari zaka hiyo iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu, kama Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Mose. 42Ile nusu waliopewa Waisraeli, ambayo Mose aliitenga na ile nusu waliyopewa wanajeshi waliokwenda vitani, 43ilikuwa kondoo 337,500, 44ng’ombe 36,000, 45punda 30,500, 46na watu 16,000. 47Kutoka nusu hii waliyopewa Waisraeli, Mose alitwaa mmoja kati ya kila mateka hamsini na wanyama hamsini, kama alivyoamriwa na Mwenyezi Mungu, akawapa Walawi ambao walihudumu katika hema la Mwenyezi Mungu.

  • Marejeo: Hesabu 31:25
  • Imechapishwa: 02/02/2020