Zakaah juu ya mkopo wa benki

Swali: Ikiwa mshahara wangu umecheleweshwa na sina uwezo mwingine isipokuwa mkopo wa benki ulio na ribaa, je, inafaa kwangu kutoa zakaah kwa pesa hizo au nisubiri mpaka nitapopokea mshahara wangu?

Jibu: Haijuzu kabisa kuchukua mkopo benki ulio na nyongeza ya ribaa. Muda wa kuwa uko na ribaa ni haramu. Ni vipi basi utatolewa zakaah?

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/28-29)
  • Imechapishwa: 01/05/2026