Yahyaa al-Hajuuriy ni mpotevu na anawatia watu mashaka katika ´Aqiydah yao

Swali: Kuna mwalimu aliwaambia wanafunzi wake maneno yafuatayo:

“Allaah amelingana juu ya ´Arshi Yake pasi na kuigusa halafu akajirudi.”

Akasema tena:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikosea katika kisa aliyekunja kipaji na akageuka kisha akajirudi.”

Akasema tena:

“Amemmnasibishia Shaykh-ul-Islaam [Ibn Taymiyyah] maoni ya Tasalsul kisha akajirudi.”

Vivyo hivyo ana makosa mengi ambayo anajirudi hapa na hapa. Je, mtu asome kwa Shaykh kama huyu?

Jibu: Huyu ni mwenye mashaka. Huyu anawatia watu mashaka katika mambo ya ´Aqiydah yao. Haijuzu kusoma kwake wala kuchukua elimu kutoka kwake. Kwa kuwa huyu ni katika wapotevu. Anawatia watu mashaka na anadhihrisha ´Aqiydah yake batili. Pale anapoona watu wanamkemea ndipo anajifanya kuwa anajirudi kihadaa. Haijuzu kumkubalia mtu huyu wala kusoma kwake. Bali ni wajibu kutahadhari naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=Snc73LjWfPE&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 26/10/2016