Swali: Kuna mwanaume ana tatizo la kutokwa hovyo na mkojo. Wakati wa swalah unapoingia na nikatawadha, baada ya kutawadha hutoka mkojo usiozidi matone mawili, naye anapata wasiwasi kwa hilo.
Jibu: Ikitoka kitu chochote, anarudia kujisafisha kwa maji na anarudia kutawadha. Aache wasiwasi. Asiharakishe, kwanza ajisafishe vizuri kwa maji, kisha akimaliza kujisafisha kwa maji, asimame na atawadhe na aache wasiwasi. Aidha aoshe sehemu zilizo karibu na tupu yake kwa maji baada ya kutawadha ili yale yanayotokana na wasiwasi ayachukulie kuwa ni yale maji aliyoyanyunyiza. Baada ya hapo jambo hilo huisha na humwondokea. Lakini ikiwa baada ya hapo bado kitamtoka kitu, basi anarudia kujisafisha, anarudia kutawadha na aoshe kilichoathirika katika nguo yake au suruwali yake. Kisha aache wasiwasi, aukate kabisa, ajishughulishe na mambo yake na ajiepushe na wasiwasi huo ili asichochewe na shaytwaan na ili shaytwaan asimchezee.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1807/حكم-وضوء-من-به-سلس-في-البول
- Imechapishwa: 04/07/2026
Swali: Kuna mwanaume ana tatizo la kutokwa hovyo na mkojo. Wakati wa swalah unapoingia na nikatawadha, baada ya kutawadha hutoka mkojo usiozidi matone mawili, naye anapata wasiwasi kwa hilo.
Jibu: Ikitoka kitu chochote, anarudia kujisafisha kwa maji na anarudia kutawadha. Aache wasiwasi. Asiharakishe, kwanza ajisafishe vizuri kwa maji, kisha akimaliza kujisafisha kwa maji, asimame na atawadhe na aache wasiwasi. Aidha aoshe sehemu zilizo karibu na tupu yake kwa maji baada ya kutawadha ili yale yanayotokana na wasiwasi ayachukulie kuwa ni yale maji aliyoyanyunyiza. Baada ya hapo jambo hilo huisha na humwondokea. Lakini ikiwa baada ya hapo bado kitamtoka kitu, basi anarudia kujisafisha, anarudia kutawadha na aoshe kilichoathirika katika nguo yake au suruwali yake. Kisha aache wasiwasi, aukate kabisa, ajishughulishe na mambo yake na ajiepushe na wasiwasi huo ili asichochewe na shaytwaan na ili shaytwaan asimchezee.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1807/حكم-وضوء-من-به-سلس-في-البول
Imechapishwa: 04/07/2026
https://firqatunnajia.com/wudhuu-wa-anayetokwa-hovyo-na-mkojo/