Swali: Kuna mtu alikuwa anavuta sigara kisha akaiacha kwa muda na akaazimia kwamba hatovuta tena, kisha akaapa kiapo kwamba akirudia kuinywa basi atafunga miaka mitatu. Baadaye akarudia tena akaivuta. Ni ipi hukumu ya kufunga ile miaka mitatu aliyojilazimisha?
Jibu: Inamlazimu atubu kwa Allaah na inamlazimu kutoa kafara ya kiapo. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kufunga milele. Hii ni aina ya kufunga mfululizo. Bali anapaswa kuwalisha chakula masikini kumi au kuwavika nguo na hiyo itamtosheleza kwa kiapo chake. Aidha inamlazimu atubu kwa Allaah na asirudie tena kuvuta sigara, kwa sababu madhara yake ni mengi, nayo ni kitu kichafu kilichoharamishwa. Hivyo inamlazimu atubu kwa Allaah, asirudie tena na atoe kafara ya kiapo kwa sababu ya kuapa kwamba hatovuta. Kama imetokea amevuta basi juu yake ni kafara ya kiapo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1790/حكم-من-حلف-ان-يصوم-ثلاث-سنين-ان-عاد-للدخان
- Imechapishwa: 04/07/2026
Swali: Kuna mtu alikuwa anavuta sigara kisha akaiacha kwa muda na akaazimia kwamba hatovuta tena, kisha akaapa kiapo kwamba akirudia kuinywa basi atafunga miaka mitatu. Baadaye akarudia tena akaivuta. Ni ipi hukumu ya kufunga ile miaka mitatu aliyojilazimisha?
Jibu: Inamlazimu atubu kwa Allaah na inamlazimu kutoa kafara ya kiapo. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kufunga milele. Hii ni aina ya kufunga mfululizo. Bali anapaswa kuwalisha chakula masikini kumi au kuwavika nguo na hiyo itamtosheleza kwa kiapo chake. Aidha inamlazimu atubu kwa Allaah na asirudie tena kuvuta sigara, kwa sababu madhara yake ni mengi, nayo ni kitu kichafu kilichoharamishwa. Hivyo inamlazimu atubu kwa Allaah, asirudie tena na atoe kafara ya kiapo kwa sababu ya kuapa kwamba hatovuta. Kama imetokea amevuta basi juu yake ni kafara ya kiapo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1790/حكم-من-حلف-ان-يصوم-ثلاث-سنين-ان-عاد-للدخان
Imechapishwa: 04/07/2026
https://firqatunnajia.com/ameapa-akirudi-kuvuta-sifara-basi-atafunga-miaka-mitatu/