Swali: Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akirudisha salamu kwa ishara hali ya kuwa yuko ndani ya swalah. Je, hilo limefutwa kwa Hadiyth au kwa Aayah?
Jibu: Hapana, halijafutwa. Mswaliji hurudisha salamu kwa ishara. Akikusalimia mtu basi unamrudishia kwa ishara; hivi kwa mkono wako, kama unavyoshikana mikono au kwa kichwa chako. Hakuna tatizo. Mtume alikuwa akiwajibu kwa ishara. Alikuwa akifanya hivi kwa mkono wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kiganja chake kikiwa kuelekea ardhini na mgongo wa kiganja kuelekea juu, kana kwamba anashikana mikono, ishara ya kurudisha salamu.
Swali: Inasemekana kuwa alifungua mlango hali ya kuwa anaswali. Je, hili ni sahihi?
Jibu: Ndio, ndio, kutokana na haja. Kidogo tu hapana tatizo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1817/كيفية-رد-السلام-في-الصلاة
- Imechapishwa: 04/07/2026
Swali: Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akirudisha salamu kwa ishara hali ya kuwa yuko ndani ya swalah. Je, hilo limefutwa kwa Hadiyth au kwa Aayah?
Jibu: Hapana, halijafutwa. Mswaliji hurudisha salamu kwa ishara. Akikusalimia mtu basi unamrudishia kwa ishara; hivi kwa mkono wako, kama unavyoshikana mikono au kwa kichwa chako. Hakuna tatizo. Mtume alikuwa akiwajibu kwa ishara. Alikuwa akifanya hivi kwa mkono wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kiganja chake kikiwa kuelekea ardhini na mgongo wa kiganja kuelekea juu, kana kwamba anashikana mikono, ishara ya kurudisha salamu.
Swali: Inasemekana kuwa alifungua mlango hali ya kuwa anaswali. Je, hili ni sahihi?
Jibu: Ndio, ndio, kutokana na haja. Kidogo tu hapana tatizo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1817/كيفية-رد-السلام-في-الصلاة
Imechapishwa: 04/07/2026
https://firqatunnajia.com/mtume-akifungua-mlango-ndani-ya-swalah/