Amemtaliki mke wake mara mbili kisha akamfananisha na mama yake

Swali: Mwanaume amemtaliki mke wake bila kumtoa katika nyumba, akamtaliki mara ya pili bila kumtoa pia, kisha akamrejea. Baadaye akajiharamishia naye kwa kumfananisha na mama yake na dada yake. Naye ni mwanaume aliyekatwa kiungo na umri wake ni wa miaka sitini na mitano na ni mkimbizi ambaye hana jamaa yeyote. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Anatakiwa atubie kwa Allaah na anatakiwa atekeleze kafara ya kumfananisha mke na mama yake. Amekwishatoa talaka mbili na amebakiwa na talaka moja. Basi anatakiwa atekeleze kafara ya kumfananisha mke na mama yake, kama alivyoamrisha Allaah, nayo ni kumuacha huru mtumwa muumini. Asipoweza, basi afunge miezi miwili mfululizo kabla hajamwingilia. Asipoweza, basi awalishe chakula masikini sitini, yaani masikini sitini, sawa na pishi thelathini, kila mmoja apewe nusu pishi ya tende au pishi ya chakula cha nchi kinacholiwa sana, mchele, ngano au shayiri. Awape masikini sitini pishi thelathini ambapo kila mmoja atampa nusu pishi kabla ya hayamwingilia.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1891/رجل-طلق-زوجته-مرتين-ثم-ظاهرها
  • Imechapishwa: 04/07/2026