Wudhuu´ umechenguka katika mzunguko wa tano katika Nyumba

Swali: Kuna mtu wudhuu´ wake ulichenguka wakati alipokuwa anafanya mzunguko wa tano kwenye Nyumba. Je, atawadhe upya na aanze kutufu upya?

Jibu: Ndio, kwa sababu Twawaaf yake imebatilika. Mizunguko yake ya kabla imebatilika kwa kuchenguka kwa wudhuu´ wake. Atawadhe na aanze kutufu upya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (91) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-22-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 12/08/2018