Swali: Masuala ya kumkufurisha kafiri yanahusiana na yule kafiri wa asili peke yake au hata yule kafiri ambaye ameritadi pia?

Jibu: Ndio. Kukufurisha ni jambo lililoenea anaingia ndani yake kafiri yule wa asili na kafiri ambaye ameritadi. Wote hawa wanataamiliwa muamala mmoja. Isipokuwa tu ni kwamba yule ambaye ameritadi anatakiwa kuambiwa atubie. Akitubia ni sawa. Vinginevyo auawe[1]. Kuhusu yule ambaye ni kafiri tokea mwanzo inafaa kufunga naye mikataba na huku akaendelea kubaki juu ya ukafiri wake. Kuhusu ambaye ameritadi haitakiwi kumwacha kwa sababu ameharibu ´Aqiydah na ameihujumu baada ya kuitambua haki. Hivyo ni wajibu kumuua kwa sababu amekuwa ni kiungo kilichoharibika.

[1] Tazama 9898

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 95
  • Imechapishwa: 21/09/2018