Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kipenzi changu wa hali ya juu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliniusia mambo matatu: kufunga siku tatu za kila mwezi, Rak´ah mbili za dhuhaa na niswali Witr kabla ya kulala.”[1]

Wasia wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapomzungumzisha mmoja katika Ummah wake basi ni kwamba amezungumzisha Ummah mzima muda wa kuwa hakuna dalili inayoonyesha kinyume chake.

Witr ni Sunnah iliyokokotezwa ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliisisitiza na akadumu juu yake, ni mamoja katika hali ya ukazi na safarini.

Uchache wa swalah ya Witr ni Rak´ah moja. Mwenye kutaka anaweza pia kuswali Rak´ah tatu, tano, saba, tisa au Rak´ah kumi na moja. Anaweza kuziswali zote kwa Tasliym moja mwishoni au akatoa Tasliym kila baada ya Rak´ah mbili.

Witr inaanza kuanzia swalah ya ´Ishaa na inaenda mpaka kupambazuke alfajiri. Yule anayepangilia kuamka mwishoni mwa usiku bora aiswali wakati huo. Vinginevyo aiswali Witr mwanzoni mwame kama ilivyotajwa katika Hadiyth hii.

[1] al-Bukhaariy (1178), Muslim (721), at-Tirmidhiy (760), an-Nasaa’iy (1677), Abu Daawuud (1433) na Ahmad (7098, 7140 na 7409).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bahjat-ul-Abraar, uk. 85-87
  • Imechapishwa: 03/03/2021