Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ

“Na wale waliotangulia wa mwanzo miongoni mwa Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema… ” (09:100)

Bi maana kuimairi njia yao. Sio kwa madai tu na kusema “mimi ni Salafiy” na kwamba “mimi nafuata njia ya Salaf.” Ukimuuliza nini maana ya njia ya Salaf:

“Sijui, lakini mimi ni Salafiy.”

Hivyo wewe sio Salafiy. Ikiwa hujui madhehebu ya Salaf wewe sio Salafiy. Vipi utakuwa pamoja na Salafiy na wewe hujui madhehebu yao?

وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ

“Na wale waliowafuata kwa ihsaan… ” (09:100)

Ikiwa unataka kuwa katika madhehebu ya Salaf, jifunze madhehebu ya Salaf na yale waliyomo, ili uweze kushikamana nayo barabara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls–14331112.mp3
  • Imechapishwa: 05/06/2020