561 – Nilimuuliza Shaykh wetu kuhusu mtu anayesema kuwa ambaye amejiharamishia mke wake anatakiwa kutoa kafara ya kiapo?

Jibu: Hapana, isipokuwa ikiwa amefanya hivyo kwa kutundika juu ya kitu, kama vile kuhimiza au kuzuia jambo. Katika hali hiyo anatakiwa kutoa kafara ya kiapo. Lakini ikiwa amesema tu “Wewe kwangu ni haramu” bila masharti yoyote, basi huko ni kumfananisha mke na mama.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 194
  • Imechapishwa: 12/03/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´