Waunge jamaa zako kwa kadiri unavoweza

Swali: Ninajua vizuri kabisa kuwa kukata uhusiano wa jamaa ni haramu. Lakini katika tabia yangu si wa kutembelea sana, jambo ambalo hunifanya wakati mwingine nisiwatembelee jamaa zangu kwa zaidi ya mwezi. Lakini sina nia mbaya kwa hilo. Je, nina dhambi kwa kufanya hivyo?

Jibu: Kilicho juu yako ni kufanya unachoweza na hakuna dhambi juu yako katika hilo. Kilicho juu yako ni jitihada kulingana na uwezo wako: kama ni kuwatembelea kadiri unavyoweza, kuwasiliana kwa simu, kwa kuandika, kwa ujumbe au kwa kuwausia wengine kuwafikishia salamu zako – kila mmoja kulingana na uwezo wake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3311/صلة-الارحام-بقدر-الاستطاعة
  • Imechapishwa: 13/08/2026