Swali: Imetokea mgogoro kati yangu na mmoja wa ami zangu kwa jambo lisilostahili kukasirikia. Matokeo yake akatoka na kutuacha na haturudishii salamu sisi sote – mimi, baba yangu na ndugu zangu – na akatukata kabisa mpaka akasafiri kwenda nchi nyingine upande wa magharibi. Haya yametokea takriban miaka mitatu iliyopita. Tufanye nini?

Jibu: Ikiwa kukatika kwake kumetokana na sababu ya jambo la Shari´ah mlilomfanyia, basi hilo halikudhuru. Yeye ndiye mkataji. Lakini fanyeni yale mnayoweza kuwasiliana naye, kumlingania katika kheri, kumtumia zawadi na kumsaidia. Huenda Allaah akamfungulia na kuuongoza moyo wake mpaka arudi. Yule anayekata uhusiano bila sababu ya kidini ndiye mkataji. Lakini nyinyi msiwe kama yeye. Muunganishe uhusiano naye na mfanyeni wema, hata kama ni kwa njia ya barua, ujumbe au simu. Mlinganieni katika kheri na mumpe nasaha “Kwa nini umefanya hivi, ee ndugu yangu? Ni sababu gani? Mche Allaah, jua kuwa Allaah anakutazama.” Apewe nasaha kwa njia ya maandishi, simu au kwa kumtembelea mmoja wenu mahali alipo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3306/بذل-الجهد-في-صلة-الرحم
  • Imechapishwa: 13/08/2026