Namna umri unavyoongezwa kwa mtu kuwaunga ndugu zake

Swali:

“Yeyote anayependa kupanuliwa riziki yake na kuongezewa umri wake, basi na awaunge jamaa zake.”

Ni nini maana ya Hadiyth hii? Na vipi umri unaongezeka kwa mwenye kuunga uhusiano wa jamaa ilihali katika Hadiyth inasema kuwa umri wa mwanaadamu huandikwa akiwa tumboni mwa mama yake?

Jibu: Tumeshatangulia kutaja hili kuhusu Hadiyth hii Swahiyh. Maana yake ni kwamba Allaah (Ta´ala) amekwishakujua tangu mwanzo kuwa huyu ambaye ataunganisha jamaa zake ataurefusha umri wake na kumpanulia riziki yake kwa sababu ya tendo hilo la kuunganisha uhusiano. Mwingine kinyume chake. Kila kitu kiko kwa makadirio ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa hiyo mwanadamu anatakiwa kufanya sababu na mambo yote yamekwishakadiriwa. Allaah amesisitiza juu ya sababu alizoziweka katika Shari´ah na kuamrisha. Tayari imepita katika ujuzi Wake ni nani atafanya na nani hatafanya.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3318/معنى-حديث-من-سره-ان-يبسط-له-في-رزقه
  • Imechapishwa: 13/08/2026