Wajulie hali kwa simu ndugu usioweza kuwatembelea

Swali: Je, inatosha kuwasiliana na jamaa kwa simu bila kwenda kuwatembelea, kwa kuwa nina udhuru kwamba mama yangu anaishi nami na ni mzee na ni vigumu kumwacha peke yake nyumbani?

Jibu: Ndiyo, inatosha. Wasiliana nao kwa simu, uliza hali zao na watumie yale wanayohitaji ikiwa wana haja. Ikiwa una udhuru, basi hilo linakutosha. Si lazima kwenda kwa miguu ikiwa hilo haliwezekani. Mawasiliano kwa kuandika, ujumbe au simu yanachukua nafasi ya matembezi ya ana kwa ana pale inaposhindikana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3307/الاتصال-بالهاتف-من-صلة-الارحام
  • Imechapishwa: 13/08/2026