Swali: Je, dada walionyonya pamoja ni katika jamaa wa kuungwa ambao ninapaswa kuwaunga?
Jibu: Hao si katika jamaa wa damu ( الأرحام). Dada wa kunyonya pamoja si katika jamaa wa damu. Jamaa wa damu ni wale wa ukoo wa damu. Vivyo hivyo baba wa mke, ndugu wa mke, ami wa mke na jamaa zake. Hawa huitwa wakwe, si jamaa wa damu. Hata hivyo inatakiwa kuwafanyia wema na kuwaunga kwa njia ya wema na kwa kulipa wema kwa wema, si kwa sababu ni jamaa wa damu. Bali kwa sababu ni uhusiano wa ndoa au kuchangia ziwa. Ukiwafanyia wema na kuwaunganisha, hilo ni katika maadili mema.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3314/الاخوات-من-الرضاعة-لسن-ارحاما
- Imechapishwa: 13/08/2026
Swali: Je, dada walionyonya pamoja ni katika jamaa wa kuungwa ambao ninapaswa kuwaunga?
Jibu: Hao si katika jamaa wa damu ( الأرحام). Dada wa kunyonya pamoja si katika jamaa wa damu. Jamaa wa damu ni wale wa ukoo wa damu. Vivyo hivyo baba wa mke, ndugu wa mke, ami wa mke na jamaa zake. Hawa huitwa wakwe, si jamaa wa damu. Hata hivyo inatakiwa kuwafanyia wema na kuwaunga kwa njia ya wema na kwa kulipa wema kwa wema, si kwa sababu ni jamaa wa damu. Bali kwa sababu ni uhusiano wa ndoa au kuchangia ziwa. Ukiwafanyia wema na kuwaunganisha, hilo ni katika maadili mema.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3314/الاخوات-من-الرضاعة-لسن-ارحاما
Imechapishwa: 13/08/2026
https://firqatunnajia.com/ndugu-wa-kunyonya-pamoja-na-ni-katika-ndugu-wanaopaswa-kuungwa/