Watu wote uchi siku ya Qiyaamah

Swali: Je, waumini siku ya Qiyaamah watakuwa wamevishwa mavazi au uchi katika kisimamo hichi?

Jibu: Watakuwa uchi. Mtu wa kwanza kuvishwa nguo atakuwa Ibraahiym (´alayhis-Salaam).

Swali: Je, waumini pia hawatokula wala kunywa katika siku hii kuu?

Jibu: Watu watakuwa wameshughulishwa na mahangaiko makubwa. Msaada unaombwa kutoka kwa Allaah. Kuhusu ni lini watavishwa nguo Allaah ndiye mjuzi zaidi. Lakini mtu wa kwanza kuvishwa nguo ni Ibraahiym kisha watavishwa nguo waumini wengine na Mitume. Lakini hayo yatafanyika lini? Allaah ndiye mjuzi zaidi. Je, ni katikati ya mchana au ni pale watapoingia Peponi? Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24365/متى-يكسى%C2%A0المومنون-يوم-القيامة
  • Imechapishwa: 03/10/2024