Vipi kuoanisha ugeni wa Uislamu na kuwepo kundi lililonusuriwa?

Swali: Vipi kuoanisha kati ya Hadiyth inayosema:

”Uislamu umeanza ni mgeni na utarudi kuwa mgeni… ”

na:

”Hatokuacha kuwepo kikundi kutoka katika ummah wangu hali ya kuwa ni chenye kushinda juu ya haki. Hakitodhurika na wale wenye kuwakosesha nusura wala wale wenye kwenda kinyume nao mpaka ifike amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) wakiwa katika hali hiyo.”[1]

Jibu: Hakuna mgongano. Utakuwa ni mgeni na wakati huohuo kutakuwepo kundi lenye kunusuriwa. Utakuwa ni mgeni na wakati huohuo kutakuwepo kundi lenye kunusuriwa lipo. Hata hivyo ni wachahe ukilinganisha na wingi wa waovu.

[1] Muslim (1920).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24358/معنى-لا-تزال-طاىفة-مع-غربة-الاسلام
  • Imechapishwa: 03/10/2024