Watu wa Makkah kupunguza swalah

Swali: Watu wa Makkah kuhusu kupunguza swalah kwa ajili ya ´ibaadah?

Jibu: Wanafuata mahujaji, kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakubalia na hakuwakataza. Hakusema:

“Enyi watu wa Makkah, timizeni swalah.”

Kama alivyowaambia siku ya ufunguzi wa Makkah:

“Timizeni [swalah zenu], kwa kuwa sisi ni wasafiri.”

Swali: Ikiwa wako mbali na msikiti wa al-Namirah na hawawezi kusikia Khutbah?

Jibu: Wataswali wenyewe Dhuhr na ´Aswr kwa pamoja majumbani mwao.

Swali: Je, mmoja wao atawatolea Khutbah?

Jibu: Ikiwa mmoja wao atawakhutubia, basi hakuna tatizo. Na ikiwa watasikiliza kupitia vipaza sauti au redio, ni sawa.

Swali: Je, maneno ya baadhi ya wanazuoni kwamba kupunguza swalah kwa watu wa Makkah ni kwa sababu ya safari yana mashiko?

Jibu: Hapana, hayakupokelewa, kwa sababu baina ya Minaa na Makkah si umbali wa safari.  Umbali wa Minaa na ´Arafah ni safari fupi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25000/حكم-قصر-اهل-مكة-للصلاة-والنسك
  • Imechapishwa: 22/01/2025