Anayefanya Sa´y na Twawaaf kwa kupanda kipando bila ya haja

Swali: Ni kipi kinachomlazimu mtu anayepanda wakati wa Sa´y na Twawaaf bila ya haja?

Jibu: Kutufu kwake na Sa´y yake ni sahihi, kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitufu hali ya kuwa mzima. Ama kuhusu Hadiyth ya Ibn ´Abbaas inayosema kwamba alikuwa mgonjwa ndio maana akapanda, ni dhaifu. Katika cheni yake yumo Yaziyd bin Abiy Ziyaad. Sahihi ni kwamba alipanda (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kuondoa ugumu kwa watu, ili wasije wakadhurika au kumdhuru.

Swali: Mtu wa kawaida anayetufu kwa kupanda kipando bila sababu yoyote?

Jibu: Anatakiwa kufundishwa kwamba Sunnah ni kutufu kwa kutembea.

Faida nyingine tunayopata ni usafi wa ngamia na kwamba kinyesi chake na mkojo wake ni safi. Ngamia hana neno. Hata hivyo ikiwa mtu anaweza kutufu kwa kutembea, basi hiyo ndiyo Sunnah kama vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyotufu kwa kutembea.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24993/حكم-الركوب-في-السعي-والطواف-بغير-حاجة
  • Imechapishwa: 22/01/2025