Watu kukumbatiana siku ya ´Iyd baada ya swalah

Swali: Tunaona watu katika siku za ´Iyd wakikumbatiana, hata kama hawakuwa wametoka safarini, na huenda muda uliowatenganisha ni mfupi tu, kama muda wa swalah. Kisha baada ya swalah ya ´Iyd wanakumbatiana. Tunaomba ubainifu wa jambo hili.

Jibu: Hatujui kuwa kukumbatiana kuna msing; bali ni desturi tu iliyozoeleka miongoni mwa watu. Kilichosuniwa ni kumuombea mwenzako akubaliwe matendo, anapokutana na ndugu yake amuombee kukubaliwa matendo. Haya yamepokelewa kutoka kwa Salaf. Ama kukumbatiana kwa sababu hii maalum, hatujui kuwa kuna msingi, bali ni desturi tu ya watu. Kwa hiyo lililo bora zaidi ni kusalimiana kwa kushikana mikono na hilo linatosha wakati wa kukutana. Asalimiane na ndugu yake kwa kushikana mikono na amwambie: ”Allaah akubariki katika ´Iyd hii”, ”Allaah anikubalie kutoka kwangu na kwako” au maneno mengine yanayofanana na hayo. Hilo halina tatizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1533/حكم-المعانقة-في-الاعياد
  • Imechapishwa: 26/06/2026