Swali: Je, mtu hubaki katika twahara kwa muda gani akiwa ametwaharika kwa njia ya kupaka juu ya soksi za ngozi?
Jibu: Ikiwa mtu amevaa soksi za ngozi juu ya twahara, kisha akapatwa na hadathi, halafu akatwaharika kwa kupaka juu ya soksi ya ngozi, kisha akazivua soksi za ngozi hizo, basi twahara yake hubatilika. Hii ni kwa sababu soksi za ngozi ni sharti la kuendelea kwa twahara hiyo. Akizivua, twahara inabatilika. Hivi ndivo wanavoona jopo kubwa la wanazuoni. Kwa hiyo soksi za ngozi zinapaswa kubaki miguuni hadi amalize muda wa kupaka. Iwapo atataka kuzivua kabla ya kuisha muda, hakuna tatizo kuzivua, lakini ni lazima arudie twahara upya. Hawezi kubaki juu ya twahara ile ya kupaka baada ya kuzivua soksi ya ngozi, ikiwa tayari alikuwa amepatwa na hadathi. Lakini ikiwa alivaa soksi za ngozi juu ya twahara, kisha akazivua kabla ya kupata hadathi, basi hakuna tatizo na twahara yake inabaki kuwa sahihi. Lakini akipata hadathi, kisha akatwaharika na kupaka juu ya soksi, halafu akazivua, basi twahara yake hubatilika kwa mujibu wa wanazuoni wengi, na hili liko karibu na maafikiano.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1538/حكم-المسح-على-الخفين-بعد-خلعهما-بعد-المسح
- Imechapishwa: 26/06/2026
Swali: Je, mtu hubaki katika twahara kwa muda gani akiwa ametwaharika kwa njia ya kupaka juu ya soksi za ngozi?
Jibu: Ikiwa mtu amevaa soksi za ngozi juu ya twahara, kisha akapatwa na hadathi, halafu akatwaharika kwa kupaka juu ya soksi ya ngozi, kisha akazivua soksi za ngozi hizo, basi twahara yake hubatilika. Hii ni kwa sababu soksi za ngozi ni sharti la kuendelea kwa twahara hiyo. Akizivua, twahara inabatilika. Hivi ndivo wanavoona jopo kubwa la wanazuoni. Kwa hiyo soksi za ngozi zinapaswa kubaki miguuni hadi amalize muda wa kupaka. Iwapo atataka kuzivua kabla ya kuisha muda, hakuna tatizo kuzivua, lakini ni lazima arudie twahara upya. Hawezi kubaki juu ya twahara ile ya kupaka baada ya kuzivua soksi ya ngozi, ikiwa tayari alikuwa amepatwa na hadathi. Lakini ikiwa alivaa soksi za ngozi juu ya twahara, kisha akazivua kabla ya kupata hadathi, basi hakuna tatizo na twahara yake inabaki kuwa sahihi. Lakini akipata hadathi, kisha akatwaharika na kupaka juu ya soksi, halafu akazivua, basi twahara yake hubatilika kwa mujibu wa wanazuoni wengi, na hili liko karibu na maafikiano.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1538/حكم-المسح-على-الخفين-بعد-خلعهما-بعد-المسح
Imechapishwa: 26/06/2026
https://firqatunnajia.com/maoni-ya-jopo-la-wanazuoni-kuhusu-twahara-ya-aliyevua-soksi-zake/