Makemeo ya kuacha swalah tatu za ijumaa mfululizo

Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth inayosema:

”Yeyote anayeacha ijuma tatu kwa kufuatana, basi Allaah hupiga muhuri juu ya moyo wake.”?

Jibu: Hadiyth hii ni Swahiyh. Imethibiti katika Hadiyth Swahiyh:

”Yeyote anayeacha ijuma tatu kwa kufuatana, basi Allaah hupiga muhuri juu ya moyo wake.”?

Tunamuomba Allaah atulinde.

Lililo kali zaidi kuliko hili ni lile lililotajwa katika Hadiyth iliyopokelewa na Muslim katika Hadiyth Swahiyh:

“Wakome watu kuacha swalah za ijumaa au Allaah atagonga muhuri juu ya nyoyo zao kisha watakuwa miongoni mwa waghafilikaji.”[1]

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (725).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1573/الحكم-على-حديث-من-ترك-ثلاث-جمع-متتالية
  • Imechapishwa: 26/06/2026