Kupunguza sehemu ya kichwa wakati wa kutoka kwenye Ihraam

Swali: Je, kupunguza nywele za sehemu ya kichwa kunatosha badala ya kunyoa kichwa chote katika kutoka kwenye Ihraam ya ´Umrah?

Jibu: Haifai. Inapaswa nywele zipunguzwe katika kichwa chote. Kama ilivyo katika kunyoa kichwa, iwe ni katika Hijjah au ´Umrah, vivyo hivyo katika kupunguza nywele, inapaswa kuhusisha kichwa chote. Haya ndio maoni ya kikosi cha wanazuoni na ndiyo yaliyo wazi zaidi kwa mujibu wa dalili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1613/حكم-تقصير-بعض-الراس-عند-التحلل-من-العمرة
  • Imechapishwa: 26/06/2026