Waswaliji msikitini kukubaliana kuchelewesha Tarawiyh

Swali: Vipi endapo kikosi cha watu watakubaliana kuswali pamoja mwishoni mwa usiku badala ya kuswali na wengine mwanzoni mwa usiku?

Jibu: Bora ni kuswali na wengine misikitini, kwa sababu imekuwa ni nembo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha watu baada ya ´Ishaa kwa sababu ni kuwafanyia upole watu.

Swali: Vipi ikiwa maamuma watakubaliana na imamu kuichelewesha swalah mwishoni mwa usiku?

Jibu: Hapana vibaya ikiwa wanaishi katika kijiji, kwa sababu mwisho wa usiku ndio bora. Lakini kuna uwezekano ipo misikiti na kuwatia ugumu watu. Watu wanaigizana na hivyo inakuwa ni kuwatia watu ugumu…

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23813/حكم-تاخير-جماعة-للتراويح-الى-اخر-الليل
  • Imechapishwa: 05/05/2024