Wasichana wa mwanamke ni Mahram wa mume ambaye si baba yao?

Swali: Mwanamke aliyeachika akiolewa na mume mwingine ambapo akamzalia watoto wa kike. Je, yule mume wa kwanza ni Mahram juu ya watoto wake wa kike ambaye kazaa na yule mume wa pili?

Jibu: Ndio, ni Mahram wao. Mwanamke akiachika na akaolewa na mume mwingine ambapo wakazaa naye wasichana, basi yule mume wa kwanza ni Mahram wa wale watoto wake wa kike ambaye kazaa na mume wake wa pili. Kadhalika endapo mwanamke huyu atakuwa na wasichana kutoka kwa mume aliyetangulia ambapo akaolewa na mume mwingine, basi huyu mume wake wa pili – ambaye ndiye yuko naye sasa – inafaa kwa wale wasichana ambaye kazaa na mume wa kwanza kufunua nyuso zao mbele yake. Kwa hiyo wasichana wa mwanamke ni Mahram wa mume ambaye si baba yao. Ni mamoja baba huyo akawa alitangulia au ndiye huyu wa sasa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1121
  • Imechapishwa: 21/04/2019