Washirikina hawa ni waovu zaidi kuliko wa kale

Swali: Ni ipi hukumu ya msemo wa mwenye kusema ´walii anaumba`?

Jibu: Huyu ni mshirikina. Mwenye kudai ya kwamba kuna mwenye kuumba pamoja na Allaah ni mshirikina amefanya shirki ambayo haikufanywa na Abu Jahl na Abu Lahab. Hakuna yeyote katika washirikina aliyedai kuwa kuna mwenye kuumba pamoja na Allaah.

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ

“Ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi, na akatiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” (29:61)

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ

“Ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” bila shaka watasema: “Allaah.” (31:25)

Huu amefikia upeo wa shirki ambao haukufikia washirikina waliokuwepo hapo mwanzoni – tunaomba Allaah atulinde.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-1-30.mp3
  • Imechapishwa: 11/08/2020