Vyote vilivyopo duniani vimeumbwa na Allaah

Swali: Mambo ya uvumbuzi ya leo kama simu, kompyuta na vinginevyo vinaingia katika viumbe vya Allaah (Jalla wa ´Alaa)?

Jibu: Hakuna kitu isipokuwa kimeumbwa na Allaah (Jalla wa ´Alaa).

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ

“Allaah ni Muumbaji wa kila kitu, Naye juu ya kila jambo ni Mtegemewa.” (39:62)

وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ

“… na hali Allaah amekuumbeni na yale [yote] mnayoyafanya?” (37:96)

Allaah ndiye Amemuumba muhandisi na mtengenezaji na kile kinachotengenezwa. Vyote ni viumbe vya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hakuna kitu kinachotoka katika uumbaji wa Allaah (Jalla wa ´Alaa).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-1-30.mp3
  • Imechapishwa: 11/08/2020