Swali:Tunawaona watu wengi wanaweka mikono yao chini ya vitovu vyao, wengine wanaiweka juu ya vifua vyao na wanawakemea kwa ukali wale wanaoiweka chini ya kitovu vyao. Wako wengine ambao wanaiweka chini ya ndevu zao. Baadhi ya wengine wanaiachia. Ni yepi ya sawa katika hayo?

Jibu: Sunnah Swahiyh imejulisha kwamba bora kwa mswaliji pindi anapokuwa amesimama ndani ya swalah basi aweke kiganja chake cha kulia juu ya kiganja chake cha kushoto juu ya kifua. Ni mamoja kabla na baada ya Rukuu´. Hayo yamethibiti katika Hadiyth ya Waail bin Hujr na Qabiyswah bin Halab at-Twaaiy kutoka kwa baba (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Pia kumethibiti yanayojulisha juu ya hilo kupitia kwa Sahl bin Sa´d as-Saa´idiy (Radhiya Allaahu ´anh).

Kuhusu kuiweka chini ya kitovu kumepokelewa juu yake Hadiyth dhaifu kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh).

Kuhusu kuiachia au kuiweka chini ya ndevu ni jambo linalokwenda kinyume na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/98)
  • Imechapishwa: 13/10/2021