Ni ipi hukumu ya kikao cha mapumziko? II


Swali: Watu katika ndugu wanatilia umuhimu kikao cha mapumziko (جلسة الاستراحة)[1] na wanawakemea wale wanaokiacha. Ni ipi hukumu yake? Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa imamu na maamuma kama ambavo imewekwa katika Shari´ah kwa anayeswali peke yake?

Jibu: Kikao cha mapumziko kimependekezwa kwa imamu, maamuma na anayeswali peke yake. Ni miongoni mwa aina za kikao kati ya Sujuud mbili. Ni kikao chepesi ambacho hakukusuniwa ndani yake Dhikr wala du´aa. Hapana neno kwa mwenye kukiacha. Haidyth juu yake zimethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Maalik bin Huwayrath, Abu Humayd as-Saa´idiy na kikosi cha Maswahabah wengine (Radhiya Allaahu ´anhum).

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/66-kikao-cha-kupumzika/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/99)
  • Imechapishwa: 13/10/2021