Wapenzi kwa ajili ya Allaah na si kwa ajili ya Mtume

Swali: Ni ipi hukumu ya msemo:

”Wapenzi kwa ajili ya Mtume wa Allaah?”

Jibu: Msemo huu, ijapo inanidhihirikia kuwa mwenye nayo anakusudia maana sahihi, anachokusudia ni kwamba tumekusanyika sote katika kumpenda kwetu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini hata hivyo ibara hii ni kinyume na yale yaliyopokelewa katika Sunnah. Hadiyth inasema:

”Anayependa kwa ajili ya Allaah na akachukia kwa ajili ya Allaah… ”

Kinachompasa ni yeye kusema ”wapenzi kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall).” Isitoshe msemo huu ni kuacha yale waliyokuwa wanayasema Salaf. Pengine yakapelekea katika kuchupa mpaka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kughafilika kutokana na Allaah. Kinachotambulika kwa wanazuoni wetu na kwa watu wema ni yeye kusema ”wapenzi kwa ajili ya Allaah”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Manaahiy al-Lafdhwiyyah, uk. 04-05
  • Imechapishwa: 01/07/2022