Wanyama wasiofaa kuchinjwa katika Udhhiyah na Hadiy

Swali: Kuna sharti zipi zinazotakiwa kutimia katika kichinjwa cha Hadiy na Udhhiyah?

Jibu: Ni lazima awe amesalimika na kasoro, kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”[Wanyama] wanne hawasihi katika wanyama wa Udhhiyah: Mwenye chongo linaloonekana wazi chongo lake, mwenye ugonjwa ambaye ugonjwa wake unaonekana wazi, kiguru ambaye uguru wake unaonekana wazi na mnyonge asiye na mifupa imara.”[1]

Amekataza pia kumchinja Udhhiyah mnyama aliyekatika pembe na sikio. Ni yule mnyama ambaye sehemu yake kubwa ya pembe au sikio imekatika. Ni lazima kuchunga kusalimika kwake na kasoro; ni mamoja ni mnyama wa Hadiy au Udhhiyah.

[1] Abu Dawuud (2785), at-Tirmidhiy (1530), an-Nasaa´iy (7/214) na Ibn Maajah (3144).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18208/الشروط-الواجب-توافرها-في-الاضحية-والهدي
  • Imechapishwa: 11/06/2024