Swali: Sisi tuna Suufiyyah wengi ambao ni wajinga ambao wanabaki kwenye makaburi kwa kipindi kirefu na wanatukufu kwayo na wanayaomba badala ya Allaah. Wanatumia hoja kuwafuata kichwa mchunga viongozi wa dini katika nchi ambao wengi wao ni waabudu makaburi au wanaofuata vipote vya Suufiyyah. Tunawasimamishia hoja hawaitambui. Kinyume chake wanasema kuwa sisi ni magaidi na wapetukaji mipaka. Je, watu hawa ni washirikina au wanapewa udhuru kwa ujinga wao?

Jibu: Wanapewa udhuru kwa ujinga ilihali nyinyi mnawabainishia na mnawasomea Qur-aan? Hawa wamesimamiwa na hoja na ujinga umewaondoka. Lakini hata hivyo ni wakaidi na ni wenye kuendelea. Nyinyi mmetekeleza wajibu wenu. Endeleeni kutoa nasaha huenda Allaah akawaongoza. Yapuuzeni maneno yao kwamba nyinyi ni magaidi na tuhuma nyenginezo. Yapuuzeni haya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliambiwa kuwa ni mwendawazimu, mchawi, kuhani n.k. Aliambiwa maneno mengi ilihali ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hiyo yapuuzeni maneno haya.

Kuhusu kwamba viongozi wa dini na wanachuoni wanafanya kadhalika sio hoja na hawatowafaa kitu siku ya Qiyaamah mbele ya Allaah. Amesema (Ta´ala):

وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا

“Watasema: “Mola wetu! Hakika sisi tumewatii mabwana zetu na wakuu wetu, basi wametupoteza njia.”” (33:67)

Haya hayatowafaa kitu siku ya Qiyaamah mbele ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (05) http://alfawzan.af.org.sa/node/2048
  • Imechapishwa: 27/11/2016