Tatizo ni kwamba mbabaishaji kama huyu nimeambiwa kuwa ana kitu katika elimu. Lakini hata hivyo hii ndio ile elimu ya kwenye cheti ambayo mtu anapewa shahada yenye kuonyesha kuwa ametakharuji kutoka kwenye chuo fulani na kujidai kuwa mimi ndiye mimi.

Kwa ufupisho ni kwamba ni lazima Ummah wa Kiislamu uwe na wanachuoni wenye elimu iliobobea. Hili ni jambo la lazima. Ummah kubaki tu na vurugu namna hii, hakika utakuwa uko katika khatari kubwa. Matokeo yake watu hawatonyooka katika dini yao na nyoyo zao hazitokuwa na utulivu. Itakuwa kila mmoja anakaa chini ya mti na kutoa fatwa, mwingine anakaa chini ya dari yake na kutoa fatwa na mwingine anakaa juu ya mlima na kutoa fatwa, jambo ambalo si sahihi. Ni lazima kuwepo wanachuoni walio na elimu iliyobobea na ilio imara. Elimu hiyo iwe imejengwa juu ya Qur-aan na Sunnah, akili na hekima.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/151)
  • Imechapishwa: 29/04/2024