Wanawake wenye kupiga mayowe na ukelele karibu na kaburi la Mtume

Swali: Baadhi ya wanawake wanapofika katika kaburi la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanaanza kupiga mayowe na ukelele.

Jibu: Haifai kwa wanawake kuruhusiwa kufika katika kaburi la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kaburi la mtu mwingine. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi na wale wenye kuyafanya kuwa ni mahala pa kuswalia na kuyawekea mataa.”[1]

Haijuzu kwa mwanamke kutembelea kaburi sawa ikiwa ni la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au la mtu mwingine. Wala haitakikani kuwepo mayowe wala ukelele kwenye msikiti. Ni lazima lizuiwe sawa ikiwa linatoka kwa wanaume au wanawake.

[1] Abuu Daawuud (3236), at-Tirmidhiy (320), an-Nasaa’iy (2043) na Ahmad (2030). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah” (225).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-qrran-19-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020